habari Mpya


Evariste Ndayishimiye Kumrithi Rais Pierre Nkurunziza Uchaguzi Mkuu Burundi.

Evariste Ndayishimiye (Pichani) kwa sasa ni Katibu Mkuu wa chama cha CNDD-FDD tangu Agosti 2016.

Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Waziri wa Mambo ya ndani na ulinzi wa umma.

Chama tawala cha Burundi CNDD-FDD, kimemteua katibu wake mkuu kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa Burundi utakaofanyika mwezi Mei 2020.

Jenerali Evariste Ndayishimiye ameidhinishwa na chama kama mrithi wa Rais Nkurunziza wa Burundi.

Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye ameteuliwa kama mgomba wa urais katika uchaguzi utakaofanyika Mei 2020 kumrithi Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

Jenerali Ndayishimiye ameteuliwa Jumapili January 26,2020 kupeperusha bendera ya chama cha CNDD-FDD katika kikao kisicho cha kawaida kilichofanyika Gitega, mji mkuu wa kisiasa baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa tatu ya chama tawala cha CNDD-FDD.

Mwaka 2018, Rais Pierre Nkurunziza alitangaza kwamba hatasimama tena katika kinyang'anyiro cha kugombea urais baada ya kubadilisha katiba ya nchi, hatua ambayo ilionekana na wengi kama njia ya wazi ya kutaka kusalia madarakani milele.

Kuchaguliwa kwa Meja Jenerali Ndayishimiye huenda kukawa mwanzo mwema wa kuondoa machafuko ya kisiasa yaiyoshuhudiwa mwaka 2015 na kutengeneza mazingira thabiti kwa Burundi.


Post a Comment

0 Comments