habari Mpya


Bingwa Mtetezi Azam FC,Simba naYanga ndani ya 32 Bora ya Kombe la FA Tanzania.

Mabingwa watetezi, Azam FC.

Shirikisho la Soka Tanzania TFF January 10, 2020 limepanga raundi ya nne ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Katika droo ya hatua hiyo iliyopangwa kwenye ofisi za Azam TV, Tabata Jijini Dar es Salaam, Simba SC na Yanga  wameangukiwa kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,  Mwadui FC ya Shinyanga na Tanzania Prisons.

Droo hiyo hivi ndivyo ilivyopangwa ambayo mechi zake zitachezwa kuanzia Januari 24 hadi 26 mwaka huu 2020, na umehusisha timu 64 za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza, Daraja la Pili na zinazoshiriki Ligi za Mikoa.

Post a Comment

0 Comments