habari Mpya


Ajali ya Basi Shinyanga Yaua Watu Wawili na Kujeruhi 20.

Na Amosi John –RK Shinyanga.

Watu wawili wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa baada ya Basi la Kampuni ya Bright Line lenye namba za usajili T 437 DFJ lililo kuwa linatoka Jijini Mwanza kuelekea Dodoma kugongana uso kwa uso na gari aina ya Nissan Station Wagon lenye namba za usajili T 173 ANW wakati mwendesha  Pikipiki yenye namba MC.489 BVR San Lg akikwepa mwendesha baiskeli katika eneo la Isela barabara kuu ya Shinyanga kuelekea Tabora.
Ajali hiyo imetokea Jumatatu January 13,2020 majira ya saa nne asubuhi wakati basi hilo likitoka Mwanza kwenda Dodoma,gari ndogo ikitokea Tinde kuelekea Shinyanga na mwendesha pikipiki akitokea Shinyanga kuelekea Tinde.

Akitoa taarifa ya hali ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga, Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Rose Malisa amesema kuwa wamepokea miili ya marehemu wawili na majeruhi 20 na kati yao majeruhi 11 wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali zao kuendelea kuhimalika.
Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Mpanda Pikipiki aliyejulikana kwa jina moja la Saidi na abiria aliyekuwa kwenye basi aliyejulikana kwa jina la Pilly Abed (12) mwanafunzi wa Dodoma.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Shinyanga Bw.Antony Gwandu amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na amebainisha kuwa chanzo cha ajali ni baada ya Dereva wa basi kumkwepa mwendesha pikipiki.

Post a Comment

0 Comments