habari Mpya


Watu Wawili Wafariki Ziwa Victoria.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.
Watu wawili wakazi wa wilaya ya Muleba Mkoani Kagera wamefariki wakiwa kwenye shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Victoria akiwemo mwanafunzi wa darasa la 3.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amewataja watu hao kuwa ni Christian Paul miaka 28 na Robinson Juvenary miaka 10 mwanafunzi wa darasa la 3 katika shule ya Msingi Kiga na miili yao imekutwa pembezoni mwa mwalo wa Kabumbile kijiji cha Ilemela wilayani humo.
Amesema chanzo cha tukio hilo ni mtumbwi waliokuwa wakiutumia kupigwa na mawimbi na kupinduka na kwamba miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na madaktari ambapo imebainika kuwa vifo vyao vimetokana na kunywa maji mengi.
Aidha Kamanda Malimi ametoa onyo kwa Wananchi hasa Wavuvi wanaofanya shughuli zao kwenye Ziwa Victoria kuzingatia maelekezo na tahadhari zinazotolewa na Mamlaka za Hali ya Hewa Nchini.

Post a Comment

0 Comments