habari Mpya


Watu watatu Wafariki Katika Matukio Matatu Tofauti Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Revocatus Malimi.

Na Anord Kailembo -RK Bukoba.

Watu watatu wamefariki katika matukio matatu tofauti mkoani Kagera likiwemo la Mwanafunzi wa darasa la 3 kukutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa kwenye kichaka.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Javan Jafety ,miaka 38 mkazi wa Nakatunga wilayani Ngara amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa kando ya njia na uchunguzi uliofanywa umembaini aliyehusika na kifo chake ni Jeremia Gwasa mwenye miaka 26.

Mwingine ni Paulin Paul  miaka 55 mkazi wa kijiji cha Igombe wilayani Bukoba amekutwa amefariki kwa kugongwa na chombo cha moto na aliyehusika na kifo hicho anatafutwa na Jeshi la Polisi

Tukio la tatu ni la mwanafunzi Evines Method mkazi wa kijiji cha Kagoma wilayani Muleba aliyetoweka nyumbani tangu December 22,2019  na kukutwa amefariki kwenye kichaka na uchunguzi juu ya kifo chake unaendelea.

Kadhalika Kamanda Malimi amewataka wakazi wa maeneo yalikotokea matukio hayo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kufanikisha uchunguzi unaondelea juu ya vifo hivyo.

Post a Comment

0 Comments