habari Mpya


Wanaume Kahama Woga wa Kuripoti Ukatili wanaofanyiwa Majumbani.

Na Faraja Marco –RK Kahama.
Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya wanaume Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga hufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini hawafiki kwenye madawati ya kijinsia kupata msaada ukilinganisha na wanawake.


Kauli hiyo imetolewa December 16,2019 mjini Kahama na Askari wa dawati la jinsia kitengo cha ukatili wa kijinsia Koplo Jane Joakimu wakati akitoa elimu ya kijinsia kwa wanaume waliofika kupata msaada kwenye dawati la jinsia.

Koplo Joakimu amesema idadi kubwa ya wanaume wanafanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kumwagiwa maji ya moto na kulazwa nje ya nyumba lakini ni wagumu kutoa taarifa kwenye vyombo husika .

Kwa upande wake John Mgara na Huruma Nasoro miongoni mwa wanaume waliotendewa vitendo vya kikatili wakizungumza na radio kwizera wamesema ni vyema madawati ya kijinsia kuwekwa  askari polisi wa kike na wa kiume ili iwe rahisi wanaume kupata msaada haraka kwa kujali usawa.

Post a Comment

0 Comments