habari Mpya


Wakulima Ngara Waandamana Wakishinikiza Kulipwa Fedha zao za Mauzo ya Kahawa.

Mkulima wa Kahawa akiwa Shambani kwake,Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera.
Na Simon Dioniz –RK Ngara.
Wakulima zaidi ya 50 kutoka vijiji mbali mbali Wilayani Ngara Mkoani Kagera wameandamana hadi ofisi za chama cha wakulima wakishinikiza kulipwa malipo ya fedha zao za mauzo ya kahawa ya msimu wa 2019 hadi 2020.
Wakizugumuza na radio kwizera December 16,2019, Wakulima hao wamedai kuwa wamelazimika kuandamana baada ya kuzungushwa kuhusu malipo yao ambapo wameshindwa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

Wamesema uongozi wa Chama cha Wakulima Ngara Farmers waliahidi kuwalipa wakulima ambapo mwisho wa malipo ilikuwa ni Novemba 21 mwaka huu lakini bado hawajalipwa jambo ambalo linalowapa wasiwasi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. David Bukozo amekiri kuwa wameshindwa kuendelea na malipo baada ya kampuni waliyoiuzia kahawa kutolipa kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments