habari Mpya


Waandishi wa Habari Radio Kwizera Washinda Tuzo ya Afya na Usafi wa Mazingira.

Waandishi wa habari  wawili wa Radio Kwizera (pichani) wamepokea  tuzo ya Afya na Usafi wa Mazingira zilizotolewa December 17,2019  kwenye  maadhimisho ya kilele cha wiki ya mazingira  yaliyofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hizo za Waandishi wa Habari walioandika na kuchapisha/kurusha habari za afya mazingira kwa kipindi cha Novemba 2018 hadi Oktoba 2019.

Bi.Auleria Gabriel na  Bw.Anord  Kailembo  wameshika nafasi  ya  wapili kwa kupata asilimia 94  katika shindano hilo ambalo liliwashirikisha waandishi wa Magazeti, Radio na Luninga.
Bi. Auleria na Bw. Kailembo wamepata ushindi huo baada ya kushirikiana kuandaa kipindi cha AFYA YAKO HAKI YAKO kilichohusu wananchi Mkoani Kagera wasiokuwa na vyoo bora.

Uandishi wa Makala za Magazeti.

Katika kundi hili, jumla ya waandishi sita (6) walituma kazi zao na kupitiwa na Kamati. Washindi kwa kundi hili ni;

Mshindi wa Kwanza: Veronica Mrema Jamvi la Habari, Dar es Salaam (97%).

Mshindi wa Pili: Shabani Njia, TESA Kahama, Kahama, Shinyanga (67%).

Waandishi wa Vipindi vya Redio.

Washiriki katika kundi hili ni sita (6) na washindi kwa kundi hili ni kama ifuatavyo:

Mshindi wa Kwanza: Idd Juma, Afya Radio Fm, Mwanza (97%).

Mshindi wa Pili: Auleria Gabriel na Anord Kailembo, Kwizera FM, Ngara, Kagera (94%).

Waandishi wa Vipindi vya Televisheni.

Katika kundi hili kazi moja tu ilitumwa ambayo iliandaliwa na waandishi wa habari wawili. Waandishi hawa ni Agnes Almasy na Peter Rogers kutoka kituo cha ITV.

Kazi ya waandishi hawa ilipata jumla ya asilimia 72 na hivyo kuibuka washindi.
Maadhimisho ya kilele cha wiki ya mazingira  yameambatana na mkutano uliowashirikisha Maafisa Afya wa mkoa ,Halmashauri na Wadau mbalimbali wa afya  yakiongozwa na  Kauli mbiu ya HUDUMA BORA ZA AFYA , MAZINGIRA NA USAFI NI KICHOCHEO MUHIMU CHA UCHUMI ENDELEVU.

Radio Kwizera inawapongeza Bi.Auleria Gabriel na Anord Kailembo kwa ushindi huo na inawashukuru wananchi wote wanaoendelea kutowa ushirikiano katika uandaaji wa vipindi ambayo ni moja ya sababu ya ushindi huo.

Post a Comment

0 Comments