habari Mpya


Uganda Mabingwa Kombe la CECAFA 2019.

Timu ya Uganda imefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge2019 kwa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Eritrea jioni ya December 19, 2019 kwenye Uwanja wa Lugogo mjini Kampala.

Ushindi huo wa taji la 15 na mara 40 jumla tangu enzi za Gossage kwa Uganda umetokana na mabao ya Bright Anukani dakika ya 31, Mustafa Kizza dakika ya 68 na Joel Madondo dakika ya 88.
Na baada ya mechi, Charles Lukwago wa The Cranes akapewa tuzo ya Kipa Bora wa Mashindano, Robel Tekle Michael wa Eritrea Mchezaji Bora na Mfungaji Bora ni Oscar Wamalwa wa Kenya.

Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Kenya iliichapa Tanzana Bara 2-1 baada ya Kenya waliokuwa mabingwa watetezi kuuachia ubingwa wa Challenge wakichapwa goli 4-1 na Eritrea.

Post a Comment

0 Comments