habari Mpya


Timu Nane Zaenda Kibishi 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Jana December 10,2019 kumechezwa mechi kadhaa za kukamilisha hatua ya makundi na timu zimefuzu hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League ambapo Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Red Bull.

Liverpool iliandaka bao la kwanza dakika ya 57 kupitia kwa Naby Keita kabla ya dakika moja mbele Mohamed Salah kufunga bao la pili dakika ya 58.

Timu za FC Barcelona, Napoli, Borussia Dortmund, Liverpool, Valencia, Chelsea, RB Leipzig na Olympique Lyon ni miongoni mwa timu ambazo zimejihakikishia kucheza hatua ya 16.

Wakati kigogo Inter Milan anaondolewa katika michuano hiyo kwa kipigo cha 2-1 kutoka kwa FC Barcelona na sasa anaenda kucheza UEFA Europa League kutokana na kumaliza nafasi ya tatu.

Post a Comment

0 Comments