habari Mpya


Taarifa ya Habari ya Saa 10 Alasiri -RK FM.

Na mwandishi wetu AMOS JOHN SHINYANGA
Baadhi ya viongozi wadini, wazee wamila na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga wameliomba Jeshi lapolisi wilayani humo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wananchi kwakuto chelewesha malalamiko yao

Hayo ya meelezwa na baadhi ya Viongozi wadini,wazee wamila na madiwani  wakati wakitoa mapendekezo yao katika kikao kilicho andaliwa na shirika la kivulini ili kupanga na kuweka mikakati ya kupambana na tatizo la vitendo vya ukatili

Wakitoa mapendekezo yao katika kikao hicho wamesema tatizo lakucheleweshwa kwa malalamiko yao ni miongoni mwa sababu zinazo wafanya wananchi kushindwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwenye maeneo yao kwa kuogopa kutumia gharama kubwa wakati wakwenda kutoa usahidi

Akijubu hoja hiyo Mrakibu mwandamizi wa Polisi mkoani Shinyanga SSP Claud Kanyorota amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na amewataka wananchi kujenga utamaduni wakutoa taarifa za baadhi ya watumisi wasiokuwa waadilifu kazini ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao
END
Na mwandishi wetu LILIAN MOLELI NGARA

Licha ya serikali kuendelea kuongeza vituo vya afya hapa nchini bado kuna baadhi ya vituo vya afya vinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa dawa na watumishi wa afya husuani katika maeneo ya vijijini
Hayo yameelezwa na baadhi wa wanachi wa kata ya Bukiriro wakati wakizungumza na Radio kwizera nakueleza kuwa kutokana na ukosefu wa dawa  katika kituo cha afya cha Bukiroro wagonjwa hulazimika kwenda kununulia dawa wenyewe huku ukosefu wa watumishi wa afya ukipelekea kucheleweshwa kwa huduma

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Bukiriro Bw. Gaston Mbeanga amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kwamba wanasubiri serikali kuajiri watumishi wengine wapya
Kituo cha afya cha Bukiriro hupokea zaidi ya wagonjwa 110 kila siku na kinahudumia zaidi ya kata 6 hali inayopelekea wagonjwa kukosa huduma stahiki kwa wakati na kituo hicho kuishiwa dawa kila wakati
END
Na mwandishi wetu ANORD KAILEMBO BUKOBA

Kwa miaka 3 mfululizo tangu idara ya afya mkoani Kagera ianze kukusanya damu kupitia kitengo cha damu salama mkoa haijawahi kufikia asilimia 50 ya makusanyo
Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dakt.Hassan Kawia ameiambia redio Kwizera kuwa mkoa wa Kagera kwa mwaka hunahitaji chupa za damu elfu 30 na kwamba kwenye makusanyo ambayo yamekuwa ya kifanyika tangu mwaka 2017 hadi 19 hawajafikia asilimia 50
Amesema kwa mwaka wa 2017 zilikusanya chupa za damu elfu 12 na mia 4 sawa na asilimia 41, mwaka 2018 zilikusanywa chupa elfu 13 na mia 5 sawa na asilimia 45 na hadi kufikia mwezi novemba mwaka huu zimekusanywa chupa elfu 12 pekee na kwamba bado uhitaji ni mkubwa

Mapema hii leo mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama na wananchi wa manisapaa ya Bukoba wakijitolea damu katika hospitali ya Rufaa ya Bukoba amewataka wana Kagera kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kunusuru maisha wa wahitaji
END
Na mwandishi wetu GIBSON MIKA GEITA
Waziri wa nishati Dakt.Medard Kaleman ametoa muda siku 23 kwa wakandarasi wa shirika la umeme nchini TANESCO kupitia mradi wa Rea kuhakikisha wanasambaza umeme katika vitongoji vyote vya Kata ya Mnekezi wilayani Chato Mkoani
Akizungumza katika  mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya kata hiyo wakati akiwasha umeme amesema  wananchi wa kata ya Mnekezi wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa nishati ya umeme kwa muda mrefu  hivyo kukosa fursa zinazopatikana zenye kuhitaji nguvu ya  umeme
Dakt.Kalemani amewataka wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kulipia kiasi cha shilingi elfu 27 ili kuanza kunufaika na umeme wa Rea ndani ya wiki moja baada ya kulipia.

Nao baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema uwepo kwa nishati ya umeme katika vijiji vyao itakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato
END

Post a Comment

0 Comments