habari Mpya


Siku 4 za Laini yako ya Simu Kutofungwa,Kaisajili Upya.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.

Zikiwa zimesalia siku chache tu (4) kufungwa kwa laini za simu nchini Tanzania, ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vodole, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya ziwa imesema kuwa licha ya wananchi wengi kupatiwa vitambulisho hivyo bado mwitikio wa wananchi kusajili laini ni mdogo.

Afisa wa TCRA kutoka ofisi ya Kanda ya ziwa Muhandisi Emmanuel Zabron amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za wenye laini za simu kitaifa ni milioni 47, elfu 63 na 602 hadi kufikia Disemba 10 mwaka huu huku line milioni 21.1 zikimilikiwa na taasisi na makampuni na kati ya hizo zilizosajiliwa kwa vidole ni milioni 19.6 sawa na asilimia 42.

Amesema kuwa Watu milioni 5, laki 5, elfu 99 na mia 610 wamepatiwa namba za vitambulisho vya taifa lakini hawajasajili laini zao na hivyo laini ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole ni milioni 21, laki 7, elfu 82 na mia 906.

Afisa msajili wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA Bw. Hassan Godigodi amesema kuwa mchakato wa utolewaji wa namba za vitambulisho unaendelea vizuri licha ya changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo ili kuhakikisha kila mlengwa anapatiwa vitambulisho.

Post a Comment

0 Comments