habari Mpya


Serikali Yabaini Miradi 159 Nchini Imekamilika Lakini Haitoi Maji .

Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso,amesema kuwa Serikali itawachukulia hatua kali wakandarasi wote waliotekeleza miradi ya maji 159 nchini ambayo imekamilika lakini haitoi maji.

Mhe.Aweso ameyasema December 19,2019 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano  Mkuu wa Mwaka wa Sekta ya Maji Tanzania Bara.

Amesema kuwa jumla ya miradi 159 ambayo ni chechefu kwani mingine imekamilika lakini haitoi maji na mingine inachukua muda mrefu kukamilika.

 Amesema kuwa unaenda  sehemu mbalimbali unakuta mradi umejengwa na tenki lipo lakini hakuna chanzo cha maji katika eneo la mradi,

 Sehemu nyingine unakuta mradi umejengwa chini ya kiwango na watalaamu wa maji wapo lakini ukiuliza utagundua kuwa fedha zimeliwa kwa kugawana mtalaamu wetu na mkandarasi,” amesema Mhe.Aweso

Aidha Mhe.Aweso amesema kuwa  wakati wa kufanya miradi ya maji kuwa  kichaka cha kuiba fedha za mradi umekwisha na atakayegundulika hata onewa huruma.
Mhe.Aweso amewataka   Wakurugenzi na Watalaamu wa Wizara kufuatilia miradi hiyo 159 ambayo ni chefuchefu na kuwachukulia hatua watalaamu wote walihusika kuhujumu fedha za serikali.

Amesema miradi 153 ipo vijijini na mingine sita ni miradi ambayo ipo mijini .

 Aidha aliwataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji kupunguza upotevu wa maji katika maeneo yao kutoka asilimia 30 iliyopo hivi sasa.

 Niwaombe  sasa tutoke maofisini twende kuangalia mitandao ya maji kama ni imara na mara nyingine taarifa zinakuja lakini mnachukua muda mrefu kutengeneza” amesisitiza Mhe.Aweso.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa hali ya huduma ya Maji nchini ni nzuri. 

Inakadiria kuwwepo takribani mita za ujazo bilioni 126 wakati mahitaji ya sasa ni mita za ujazo ni bilioni 40.

Akielezea suala la mabadiliko makubwa katika muundo wa kitaasisi wa utoaji wa huduma ya Maji nchini, Prof. Mkumbo amesema wameanzisha Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijini (RUWASA), ambayo anachukua jukumu la Mamalaka ya Serikali za mtaa katika kusiamamia miradi ya Maji na kusiamamia utoaji wa huduma.


Bw.Rashid Abdalah ambaye ni muhitimu wa shahada ya uhandisi wa rasilimali Maji na umwagiliaji ya chuo cha Maji kwa mwaka 2018/2019 amesema kuwa wanafahamu kuwa Serikali imejiwekea lengo la kufikia asilimia 85 ya upatikanaji wa huduma ya Maji vijijini na asilimia 95 kwa upande wa mijini ifikapo mwaka 2020.

Ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 inaagiza kuwa ifikapo mwaka 2020 upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wananchi ufikie asilimia 95 kwa miji mikuu ya Mikoa, asilimia 90 kwa Miji na Wilaya, Miji midogo na maeneo yanayo hudumiwa na miradi ya Maji ya kitaifa na asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini.

Post a Comment

0 Comments