habari Mpya


Rais Magufuli Aongeza Siku 20 Usajili Laini ya Simu Kwa Vidole.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisajili laini yake ya simu kwa njia ya alama za vidole mjini Chato Mkoani Geita, December 27, 2019.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli, December 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole mjini Chato mkoani Geita na kuwasisitiza Watanzania wahakikishe laini zao za simu zinasajiliwa kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Pamoja na kufanya hivyo, rais ameongeza siku 20 kuanzia January 1 hadi January 20, 2020 kwa Watanzania wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 December, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.
…Akielekea katika ofisi ya usajili wa simu.

Soma Hapa Taarifa Kamili.


Post a Comment

0 Comments