habari Mpya


NGARA: Watu watatu wafariki wakati wakichimba Madini

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele
Watu wa tatu wilayani Ngara mkoani Kagera wamefariki baada ya kukosa hewa safi wakiwa katika shimo lenye urefu wa mita 35 wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa Madini

Shimo ambalo limesababisha vifo vya wachimbaji watatu 


Tukio hilo limetokea katika kijiji cha kihinga wilayani Ngara mkoani Kageraambapo hata hivyo watu hao walio fariki wanadaiwa kuwa raia kutoka nchini jirani ya Burundi
Kufuatia tukio hilo Serikali Wilayani Ngara Mkoani Kagera imepiga marufuku na kuufunga kwa muda Mgodi wa machimbo ya madini aina ya Tine uliopo kijiji cha Kihinga kata ya Kibogora Wilayani humo kufuatia watu hao watatu kufariki kwenye machimbo hayo

Mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanal Michael Mtenjele amesema serikali imepoteza nguvu kazi ya taifa na kwamba watu wote waliokuwa wakijihusisha kwenye machimbo hayo wanatakiwa kuondoka na kuitaka wizara ya madini kufuatilia uhalali wa uwepo wa mgodi huo

Amesema ikiwa agizo hilo litapuuzwa serikali ya kijiji cha Kihinga watachukuliwa hatua na kuvitaka vyombo vya dola kumsaka mmiliki wa shimo hilo


Post a Comment

0 Comments