habari Mpya


Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Yashindwa Kuzoa Taka kwa Wakati Kisa Gari kutumiwa na Idara Nyingi.

Wananchi wakitoka kumwa taka katika kizimba hiki kilicho karibu na makazi yao.

Na Simon Dioniz – RK Ngara.

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera imesema uwezekano wa kuzoa taka zilizopo kwenye maeneo mbali mbali ya mji wa Ngara ni mdogo kwa sasa kutokana na upungufu wa Watumishi na ukosefu wa gari la kuzolea taka hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Mazingira wilaya ya Ngara Bw. Athanasio Andrew ambapo amesema kwa sasa Halmashauri itashindwa kuzoa taka zilizoko mjini kutokana na gari lililopo kutegemewa na kila idara, hivyo kuathiri shughuli hizo.
Amesema ikiwa gari litapatikana wataanza kuzoa taka hizo na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanaacha tabia ya kusambaza taka barabarani hali ambayo ni hatari kwa afya za wakazi wa maeneo hayo. Hivi karibuni wakazi wa maeneo ya Nakatunga  wilayani Ngara wamelalamikia Halmashauri hiyo kwa kushindwa kukusanya taka hasa katika kipindi hiki cha mvua na kusema kuwa ni hatari kwani nyakati za usiku hutoa harufu mbaya.

Post a Comment

0 Comments