habari Mpya


Amina Semagogwa atwaa tuzo za Shahidi wa Maji kwa mara ya pili mfululizo.


Pichani ni mwandishi Amina Semagogwa akikabidhiwa tuzo ya umahiri wa uandishi wa habari za maji na katibu mkuu wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo
Na mwandishi wetu Auleria Gabriel: 
Mwandishi wa habari wa Redio Kwizera Amina Semagogwa amejinyakulisha tuzo ya uandishi bora wa habari za Maji nchi Tanzania zinazotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa maji.

Tuzo hizo zimetolewa jana katika ukumbu wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam mgeni rasmi akiwa ni katibu mkuu wizara ya maji Prof. Kitila Mkumbo
Amina Semagogwa amepata ushindi katika vipengele viwili ambvyo ni mwandishi mwenye umri mdogo na mwandishi mahiri katika kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji na pia amekuwa mshindi wa jumla kati ya kazi 40 zilizoshindanishwa kutoka kwa waandishi 20 Tanzania bara na visiwani.
Hii ni mara ya pili kwa mwandishi Amina kupata ushindi katika kuaandaa vipindi bora vinavyohusu masuala ya maji ambapo mwaka jana pia aliibuka mshindi wa jumla na kwa mwaka huu Redio Kwizera imepatiwa tuzo ya heshima kwa kuwa na vipindi vinavyohamasisha maendeleo ya maji nchini Tanzania.


Redio Kwizera inampongeza Bi. Amina kwa ushindi huo na pia inawashukuru wasikilizaji na wananchi wote kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhabarisha umma juu ya masuala mbalimbali yaliyopo ndani ya jamii.


Akizungumza katika halfa hiyo, mratibu wa tuzo za habari za maji mwaka 2019 Bw. Kennedy Mmari amempongeza Bi Amina pamoja na kituo cha redio Kwizera kwa kuwa na vipindi bora vinavyohamasisha utunzaji wa rasilimali za maji.

Post a Comment

0 Comments