habari Mpya


Waziri Ndalichako "awapa rungu Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kupambana na Utoro Nchini.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezindua jengo jipya la Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Elimu Wilaya Misungwi mkoani Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchini Tanzania kuweka mikakati ya pamoja ya kupambana na utoro katika Shule za Msingi na Sekondari.

Waziri Prof. Ndalichako alifanya uzinduzi huo Novemba 09, 2019 ambapo ofisi hiyo ni miongoni mwa ofisi 100 za Udhibiti Ubora wa Elimu zinazojengwa katika Halmashauri mbalimbali nchini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Elimu Wilaya Misungwi mkoani Mwanza. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya Misungwi,Bw. Juma Sweda (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw.Kisena Mabuba (wa pili kushoto).

Post a Comment

0 Comments