habari Mpya


Wahitimu 22 wa Chuo cha Ufundi ICCO-Muleba Wapewa Vifaa Bure vya Ufundi.

Na Shafiru Yusuf -RK Muleba.

Mmoja wa Wanafunzi 22 wanaoishi mazingira magumu, wanaosomeshwa katika Chuo cha Ufundi cha ICCO kilichopo kijiji cha Ilemela kata ya Gwanseli Wilayani Muleba Mkoani Kagera akipokea Cherehani aliyokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera ,Mhandisi Richard Ruyango (aliyevaa kaunda suti katikati) wakati wa hafla ya kupatiwa vifaa vya ufundi vyenye thamani ya zaidi ya million 13.
Akitoa vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa huduma ya kuwasomesha watoto hao ambao wanaishi mazingira magumu ,wakiwemo yatima inawasaidia kuweza kujiajiri nakuondoa hali ya utegemezi kwa jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Jeofrey Kiletwa amesema vifaa vilivyo gawiwa kwa wahitimu hao 22 ni CHEREHANI, VITI,MEZA NA VIFAA VYA KUFANYIA KAZI ZA UFUNDI , ikiwa ni ufadhiliwa kutoka kwa Watu Swideni.

Nao baadhi ya Wahitimu waliohitimu mafunzo ya ufundi na ujasiriamali na kupatiwa vifaa hivyo, pamoja na kushukuru ,wamesema elimu waliyopewa wataitumia kubuni miradi ya kiuchumu itakayozalisha fedha ili ziwasaidie kuleta maendeleo yao ,familia na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments