habari Mpya


Waandishi Wafundwa Kuripoti kwa Kina Habari za Nishati Jadidifu Nchini.

Na Auleria Gabriel –RK Dodoma.

Waandishi wa habari 20 Tanzania kutoka kwenye vyombo vya redio, televisheni na magazeti, wamenufaika na kambi ya siku tatu ya mafunzo juu ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa kuhusu Nishati Jadidifu.

Mafunzo hayo ambayo yameanza Novemba 12 hadi Novemba 14,2019 jijini Dodoma, ni maandalizi ya awali kabla ya kuanza mafunzo kwa vitendo yatakayochukua muda wa miezi sita na yanaratibiwa na kampuni ya habari na teknolojia ya NUKTA AFRIKA ikishirikiana na shirika la HIVOS na chama cha Waandishi wa Mazingira Tanzania JET.
 
Mafunzo hayo yamejumuisha Wataalam mbalimbali waliotoa uzoefu juu ya masuala ya nishati ikiwemo TANESCO, REA, EWURA, ENERGY CHANGE LAB na ENSOL.

Pia wamepata nafasi ya kutembelea kituo kidogo cha kuzalisha umeme wa jua cha Rafiki Power katika kata ya Dongo wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ambacho kimefanikiwa kusambaza nishati ya umeme kwenye kaya 360. 
 
Nishati Jadidifu, ni nishati mbadala inayozalisha umeme, itokanayo na vyanzo asilia kama vile, mwanga wa jua, nguvu ya upepo, kinyesi, maji na joto kutoka ardhini na hudumu kwa muda mrefu.

Na inaelezwa kwamba ikiwa waandishi wa habari wataongeza jitihada katika kuripoti habari zilizopo katika sekta ya nishati jadidifu itawafungulia wananchi fursa mbalimbali ikiwemo ajira na kukuza shughuli za uchumi hasa katika maeneo ya vijijini. 
 

Post a Comment

0 Comments