habari Mpya


Simba SC Mbioni Kutumia Uwanja Wake wa Bunju December 2019.

Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuandika historia ya zaidi ya miaka 80 toka kuanzishwa kwake 1936  kwa kufanikiwa kuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unaelekea kukamilika siku za usoni.

Simba SC ilianza kujenga uwanja huo miaka kadhaa iliyopita , lakini haukwenda kwa kasi kutokana na uchumi kuwa mbaya.

Uwanja huo ambao upo Bunju , Jijini Dar es Salaam uhusisha viwanja viwili ambapo mmoja ni wa nyasi asili na mwingine wa nyasi bandia ambavyo vyote vitatumika kwa ajili ya mazoezi. 
Simba SC watatumia uwanja wa nyasi asili kwa ajili ya mechi ambazo watakuwa wanachezea kwenye viwanja vya mikoani na halikadhalika bandia endapo wakipangiwa kukipiga Uhuru Stadium ama Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa zinasema,Simba SC  wanaweza kuanza kutumia uwanja wa Bunju mapema mwezi ujao wa December 2019 na watakuwa wanaandika historia ya kuwa timu ya kwanza dhidi ya watani zao wa jadi Yanga SC iliyoanzishwa 1935 kumiliki kiwanja hicho huku Kwa wakiokoa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa siku kwa ajili ya kulipia viwanja vya kufanyia mazoezi ya timu hiyo. 
 

Post a Comment

0 Comments