habari Mpya


RC Gaguti -Awachukulia Hatua Wasimamizi Miradi ya Ukarabati Shule Kongwe Kwa Uzembe.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewaweka ndani watumishi 3 wa serikali na mkandarasi mmoja wanaosimamia baadhi ya miradi inayotekelezwa manispaa ya Bukoba.

Watumishi hao ni Mhandisi wa Majengo wa Manispaa ya Bukoba Bw.George Geofrey kutosimamia ipasavyo ukarabati huo,Mkuu wa shule ya Sekondari Kahororo Bw. Marick Omary, Makamu mkuu wa shule ya Sekondari  Bukoba,Bw.Siasa Phocus alichukuliwa hatua kwa kuzembea kusimamia ukarabati wa shule hiyo huku zaidi ya milioni 900 zikiwa zimeishatumika kati ya Shilingi bilioni 1,481,701,194.33 zilizotolewa na Serikali kuhakikisha shule hiyo inarudi katika hali nzuri na Kaimu Mhandisi wa kampuni ya Mazinga Holding Company inayohusika na ujenzi wa ukarabati wa shule ya Kahororo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi kuwaweka chini ya ulinzi wasimamizi wa miradi ya ukarabati wa Shule kongwe katika Manispaa ya Bukoba baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo na kutoridhishwa na kasi ya maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo wakati Serikali ilishatoa fedha zote za ukarabati kila shule. 
Mkuu wa Mkoa Gaguti alichukua hatua hiyo Septemba 21, 2019 wakati wa ziara yake Manispaa ya Bukoba katika Shule kongwe za Kahororo, Rugambwa, Kagemu na Bukoba ambazo kwa pamoja zilipewa jumla ya shilingi bilioni 2,595,890,485.33 na Serikali kufanya ukarabati wa majengo ili kuzirejesha shule hizo katika hali nzuri lakini pamoja fedha hizo kuingizwa katika kila akaunti ya shule husika ukarabati umechukua muda mrefu au kuendelea kwa kusuasua na kupitiliza muda uliotolewa na Serikali kukamilika. 
Shule ya Sekondari Kagemu ilipewa na Serikali Shilingi milioni 152,000,000 tayari muda wa ukarabati umeisha na zimelipwa milioni 49,485,277.22 Shule ya Sekondari Kahororo ilipewa na Serikali shilingi milioni 893,883,994 kati ya hizo zimetumika shilingi milioni 297,966,594.96 muda wa ukarabati ukiwa umeisha bila kazi kukamilika. 

Shule ya Sekondari Rugambwa ilipewa shilingi milioni 872,800,297 na zilizotumika ni shilingi milioni 275,125,889.25 ambapo muda wa ukarabati ukiwa umeisha.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa, ameagiza miradi ya ukarabati inayofanyika kwenye Shule za Sekondari Lugambwa, Kahororo na Bukoba kukamilishwa haraka ifikapo December Mwaka huu,2019 na hatotaka maelezo mengine ya kutokukamilika kwake.

Post a Comment

0 Comments