habari Mpya


Dawa za Raniplex, Rantac na Aciloc Zazuiwa Kutumika Nchini.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) inawataka wote waliokuwa wanatumia dawa za Raniplex 150 mg, Rantac 500 mg/mL na Aciloc 150 mg, ambazo hutumika kwa kiungulia na vidonda vya tumbo, kuacha mara moja na kuripoti kituo chochote cha Afya kilicho karibu.

Uamuzi huo wa TMDA unafuatia hatua ya mashirika mengi ya madawa ya kimataifa kuonya kuwa dawa hizo zinachanganywa na vitu ambavyo si salama kwa matumizi na vinavyoweza kuleta saratani, na sasa ziko katika uchunguzi. Dawa hizo huwa katika mfumo wa maji, vidonge na sindano.


Post a Comment

0 Comments