habari Mpya


Benki za CRDB na NMB Ngara Zaombwa Kusogeza Huduma Maeneo ya Vijijini.

Na Erick Ezekiel –RK Ngara.

Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani kagera limeziomba Tasisi za kifedha kuanzisha huduma ya kudumu ya kibenki katika eneo la Rulenge ili kuongeza usalama wa fedha za wananchi.

hayo yamejiri katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/2020 kilichoketi November 6 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara.

Diwani wa Kata ya Kibogora Bw.Adroniz Bulindoli amelieleza baraza kuwa wakazi wa tarafa ya rulenge mpaka sasa hulazimika kusafiri zaidi ya kilomita 45 kutoka rulenge kufuata huduma za kibenki mjini ngara hali inayotishia usalama wa fedha kutokana na kusafirishwa mkononi.

Bw.Erick Nkilamachum ni diwani wa kata ya Bukirilo amesema kuwa ipo haja ya benki zilizpo mjini Ngara kuangalia uwezekano wa kuanzisha huduma ya kudumu katika eneo kwakuwa hata fedha za serikali watendaji hulazimika kuzifarisha mkononi bila ulinzi jambo linaweza kusababisha hasara kwa serikali.
Meneja wa bank ya CRDB tawi la Ngara Bw.Herman Thomas amesema maombi hayo ya wawakilishi wananchi ni mazuri na kwamba wao wapo tayari kuanzisha huduma katika eneo hilo.
Nae Meneja wa bank ya NMB tawi la Ngara Bw.Godfrey Martin Amesema upo utaratibu wa kutuma maombi kama kuna uhitaji wa huduma hiyo ambao unatakiwa kuanzia ofisi ya mkuu wa wilaya.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael Mtenjele amesema utaratibu unaotakiwa ikiwemo kuandika barua ya maombi uanzishwaji wa tawi jipya katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge utafanyika ili huduma zianze kupatikana.

Post a Comment

0 Comments