habari Mpya


AFCON 2021 -Taifa Stars Yajipigia Equatorial Guinea Nyumbani.

Mashabiki wa Taifa Stras Uwanjani Taifa.

Timu ya Tanzania –Taifa Stars, imeanza vyema mbio za kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea, usiku wa jana november 15,2019 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, Equatorial Guinea walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mchezaji wa Sassuolo ya Italia, Pedro Mba Obiang dakika ya 15 akimtungua kipa mkongwe wa Tanzania, Juma Kaseja kwa shuti la mbali.
Kipindi cha pili, Kocha Mrundi wa Tanzania, Etienne Ndayiragije alifanya mabadiliko ya kuongeza nguvu katika safu ys ushambuliaji, akimtoa beki wa kulia Hassan Kessy na kumuingiza mshambuliaji, Ditram Nchimbi,mabadiliko yaliyoisaidia Taifa Stars kupata bao la kusawazisha likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Msuva dakika ya 68 akimalizia mpira uliookolewa na kipa baaada ya yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Taifa Stars ilipata bao la pili dakika ya 90 na ushei baada ya kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar Junior ‘Sure Boy’ kufunga bao la ushindi kwa shuti la mbali.  

Baada ya ushindi huo, Taifa Stars itasafiri kuwafuata Libya waliofungwa magoli 4-1 na Tunisia, Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir Jumanne ya Novemba 19,2019 kwa mchezo wa pili wa kundi hilo la J linaloongozwa na Tunisia alama 3,wakifuatiwa na Tanzania alama 3 huku Equatorial Guinea na Libiya wakiwa hana alama yoyote.
 

Post a Comment

0 Comments