habari Mpya


AFCON 2021 - Taifa Stars Yachapwa 2-1 na Libya.

Kushindwa kulinda goli la mapema baada ya kuwaruhusu Libya kutoka nyuma kipindi cha pili na kushinda magoli 2-1 katika mchezo wa Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 usiku wa November 19,2019 kumeifanya Tanzania kupoteza mchezo huo kwenye uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir, Tunisia.

Pamoja na kufungwa, Tanzania inaendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi J ikiizidi wastani wa mabao tu na Libya baada ya wote kufungana kwa pointi, tatu kila timu. 

Nahodha Mbwana Ally Samatta alianza kuifungia Tanzania dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti baada ya winga Simon Msuva kuangushwa na Mohamed Aleyat kwenye boksi.
Dakika ya 68, Mwamuzi alitoa penalti ya kuungaunga kwa Libya na bao likapachikwa na Sand Masoud dakika ya 68 huku dakika ya 81 zikiwa zimebaki dakika 9 mpira kukamilika Anias Saltou aliandika bao la pili akiwa ndani ya 18 kutokana na safu ya ulinzi kufanya makosa ya wazi.

Mchezaji wao tegemeo kwa Libya, Hamdou Mohamed alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87.

Mechi nyingine ya kundi hilo, Equatorial Guinea imefungwa nyumbano 1-0 na Tunisia Uwanja wa Nuevo mjini Malabo. 

Taifa Stars itarejea Tunisia Agosti 31,2020 kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza katika kundi hilo dhidi ya wenyeji, siku ambayo Libya watakuwa wenyeji wa Equatorial Guinea.

Post a Comment

0 Comments