habari Mpya


Yanga Yagoma Kuchapwa na Polisi Tanzania Ligi Kuu Bara.

Yanga SC imelazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo October 3, 2019.

Leo Yanga SC ilicheza bila kocha wake, Mkongo Mwinyi Zahera ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kufuatia tuhuma za kutoa maneno yasiyofaa baada ya mechi ya kwanza wakifungwa 1-0 na Ruvu Shooting Agosti 28,2019 hapo hapo Uwanja wa Uhuru. 

Timu iliongozwa na Kocha Msaidizi, Mzambia Noel Mwandila aliyekuwa akisaidiwa na kocha wa makipa, Manyika Peter.

Katika mchezo huo, Mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Ditram Nchimbi anayecheza kwa mkopo kutoka Azam FC akafunga mabao matatu mfululizo kuanzia dakika ya 29, 55 na 58 huku Yanga SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kuandika bao la mapema mnamo dakika ya 6 kupitia kwa Mrisho Ngassa na David Molinga aliye katika msimu wake wa kwanza akafunga kwa kichwa dakika ya 22 na dakika ya 65.

Post a Comment

0 Comments