habari Mpya


Waziri Mkuu Aagiza Watumishi Tanzania Kuandaliwa Kwa Ajili ya Maisha ya Uzeeni.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA  ameiagiza Wizara Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Wizara ya Fedha pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kuanzisha programu ya kuwaandaa watumishi wa umma nchini kujiweka tayari kwa ajili ya maisha ya uzeeni.

Waziri Mkuu amesema hayo October 01,2019 Mkoani Mtwara wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya Nnangwanda Sijaona.

Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zote nchini  kutenga bajeti  kwa ajili ya kuhudumia Wazee na kuitaka Jamii kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma kwa wazee ikiwemo Idara ya Ustawi katika ngazi ya Halmashauri na Wilaya.

Aidha Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wazee wanapatiwa huduma ya Afya iliyoboreshwa ili wazee waweze kupatiwa huduma ya Afya bure bila kubugudhiwa na mtu yeyote.

Pia Waziri Mkuu amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuomba kibali cha ajira ili kuajili Maafisa Ustawi wa Jamii wa kutosha ili waweze kutoa huduma kwa jamii ikiwemo wazee kuanzia ngazi ya Wilaya mpaka Mkoa.

Aidha ameitaka Wizara inayohusika na masuala ya wazee kuhakikisha taasisi zote Binafsi zinazojishughulisha na masuala ya wazee kuhakikisha zinatumia rasilimali zinazopatikana katika Mashirika hayo zinatumika kuwanufaisha wazee na kuachana ya kutumia fedha nyingi kwenye makongamano na semina.

Waziri Mkuu MAJALIWA ameongeza kuwa ni jukumu la kila mmoja mwenye mamlaka kuhakikisha wanafuatilia wazee ili kutambua michango yao katika Taifa lakini pia kutoa huduma kwa wazee hao ambao kimsingi wazee hawa ndio kioo cha Taifa hili.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema Tanzania kwa sasa ina Wazee takriban Milioni 2 ambayo ni asilimia 5 ya Watanzania wote huku akiongeza kuwa kila watu 100 kati yao watu ni wazee.

Waziri UMMY ameongeza kuwa Sera ya Wazee ya Mwaka 2003 na Sera ya Afya iliyopo sasa inatamka wazi kuwa huduma za matibabu bure zinatolewa kwa wazee wasiojiweza na sio kwa wazee wote kwani pamoja na kwamba wote ni wazee lakini wapo wenye uwezo ambao bado wanafanya kazi.

Waziri UMMY amefafanua kwa Wazee takriban elfu 6 wasio na uwezo tayari wamepatiwa vitambulisho bila malipo na kuhaidi kuwa Serikali itaendelea na jitihada za kuwatambua wazee hao ili kuendelea kuwapatia vitambulisho hivyo lakini pia akisema kwamba kwasasa Serikali ina jumla ya mabaraza ya wazee elfu 6 kote nchini.

Waziri UMMY  amesema Serikali kwa sasa ina jumla ya wazee 479 wasiojiweza ambao wanatunzwa na Serikali katika makazi 17 ya wazee na inaendelea kuboresha makazi hayo kwa kuyakarabati ili kuboresha miundombinu ya maji lakini pia Serikali inajipanga kupunguza makazi hayo toka 17 hadi 8 ili iweze kuja hudumia kwa ubora zaidi.

Wakati huo huo Mwenyekiti Msaidizi Mtandao wa Wazee Taifa Mzee ABDALLAH MOHAMED MAJUMBA amesisitiza utekekelezwaji wa uanzishwaji wa Sheria ya wazee na kuongeza kuwa kwa wazee wengi hapa wanatumia fursa ya  Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa kupaza sauti zao.

Post a Comment

0 Comments