habari Mpya


Wanawake Biharamulo Gombeeni Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano kuhusu Umuhimu wa Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 wilayani Biharamulo.

Na William Mpanju –RK Biharamulo.

Wanawake wilayani Biharamulo  Mkoani  Kagera  wametakiwa kujitokeza  kuchukua fomu pindi zitakapoanza kutolewa  ili waweze kugombea  nafasi mbalimbali za uongozi katika  vijiji ,mitaa na vitongoji  ili  kuondoa mfumo dume  kwenye uongozi.

 Hayo yamesemwa  na  afisa uchaguzi  wilaya ya Biharamulo  Bw Kalokola  Kasimbazi wakati akiongea na Radio Kwizera juu ya umuhimu wa wanawake  kujitokeza kugombea kwenye  hasa  uchaguzi wa serikali za mitaa  utakaofanyika  November 24 mwaka huu,2019.

Amesema  Mwanamke  mwenye  sifa anapaswa kujiamini na kuhamasisha wenzake  wamchague  kuwa kiongozi wao  katika kijiji ,mtaa na kitongoji   ili waweze kuleta mabadiliko chanya  ndani ya jamii kutokana na uadilifu walionao.

Kwa upande wao Baadhi ya wanawake wilayani Biharamulo ,wameahidi kujitokeza kuchukua fomu zitakazoanza kutolewa  October 29 hadi  November 4,Mwaka huu,2019 ili kugombea nafasi hizo.

Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 utafanyika November 24,mwaka huu,2019 na  unatoa nafasi kwa mtu yeyete mwenye sifa , kugombea .

Post a Comment

0 Comments