habari Mpya


Wananchi Nyang’hwale Waiomba Serikali Kushusha Bei ya Vifaa Vya Ujenzi ili Wajenge Vyoo Bora.

Serikali kupitia idara ya Afya wilayani Nyang’hwale mkoani Geita imetoa muda wa mwezi mmoja kwa kaya zisizo na vyoo kuhakikisha zinajenga na zile zisizo na vyoo zihakikishe zinakarabti vyoo vyao.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nyugwa, Afisa Afya wilayani Nyang’hwale Bw. Sebastian Masunga amesema sasa ni msimu wa mnvua hivyo kaya isiyo na choo inahatarisha afya za watu wake.

Bw. Masunga ameeleza kuwa kutotumia choo kwa usahihi kunasababisha uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa yatokanayo na uchafu wa mazingira kama vile kipindupindu, hivyo hawezi kumuonea aibu mtu yeyote katika suala hilo.

Kufuatia agizo hilo, Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Nyang’hwale wamesema baadhi ya kaya zinakosa vyoo bora kutokana na uhaba wa fedha za kununua vifaa vya kujengea hivyo serikali iwasaidie katika kushusha bei ya vifaa vya ujenzi madukani.

Post a Comment

0 Comments