habari Mpya


DC Ngara- Wananchi Shirikini Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili Kuchagua Viongozi Bora.

Na Mohamed Makonda –RK Ngara

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele amewaasa wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha kuwa wanashiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo kwenye maeneo yao.

Luteni Kanali Mtenjele ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi kwenye fainali ya ligi ya ngombe mnyama K9, wilayani Ngara.

 Amesisitiza kuwa  suala la uchaguzi ni la kila raia aliyejiandikisha, hivyo  muhimu Wananchi wakashiriki  uchaguzi huo ,kuliko kulalamika kuwa viongozi waliochaguliwa  wanarudisha nyuma jitihada za maendeleo.
Aidha, Luteni Kanali Mtenjele ametahadharisha tabia ya baadhi ya wagombea kupenda kutoa rushwa na baadhi ya wapiga kura kupokea na kwamba kufanya hivyo si tu kuwa ni kinyume cha sheria bali pia ni kujikosesha nafasi ya kujiletea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika nchi nzima Novemba 24, 2019  huku Wananchi milioni 19 wakijiandikisha ikilinganishwa na mwaka 2014 ambapo wananchi Milioni 11. 

Katika Fainali hiyo,Bingwa aliibuka Benaco Stars akimfunga Veteran FC bao 3-2 na kuzawadiwa Ng'ombe mnyama mwenye thamani ya shilingi Laki 5 huku Veterani FC akipewa Mbuzi mnyama mwenye thamani ya shiingi Laki Moja.

Post a Comment

0 Comments