habari Mpya


Wanafunzi Shule ya Msingi Bugoye A, Shinyanga Walia na TARURA Kuwawekewa Kivuko cha Waenda kwa Miguu.

Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Fortunatus Muslim pichani alipokuwa katika ukaguzi wa Kivuko cha waenda kwa miguu Jijini Dar es salaam na kuwataka madereva kuheshimu vivuko hivyo kwani viko kisheria na kwamba  wataendelea kuwasilisha na Mamlaka ili kuweka alama na vivuko maeneo ambapo hayaja.

Na Amos John –RK Shinyanga 89.7

Wanafunzi na Walimu wa shule ya msingi Bugoye A iliyopo Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga, wameiomba Mamlaka ya usimamizi wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  kuwawekea   kivuko cha waenda kwa Miguu katika barabara ya kuelekea kanisa katoliki ili kiwasaidie kuvuka salama barabarani.

Wakiongea na Radio Kwizera shuleni hapo,Joyce Ngeme na  Lazideus Morisi ambao ni wanafunzi wa darasa la sita, wamesema wamekuwa wakipata shida kuvuka barabara ili kuwahi vipindi shuleni.
Aidha, Kutatua changamoto hiyo ya barabara  kukosa vivuko vya waenda kwa miguu,tayari Msimamizi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ,Manispaa ya Shinyanga , Mhandisi Kulwa Maige amemuagiza Mkandarasi anayejenga barabara za mtaa, kampuni ya JASSICO kuweka alama hizo.

Post a Comment

0 Comments