habari Mpya


Wakulima Ngara Tumieni (Samadi) Kulima Msimu huu.

Mvua Ngara September 2019.

Wakulima wilayani Ngara mkoani Kagera wameshauriwa kutumia Mbolea ya Asili (Samadi) katika msimu huu wa Kilimo kutokana na mawakala wa pembejeo hizo kutofika vijijini.

Akizungumza na Radio Kwizera, Afisa Kilimo wilayani Ngara Bw.Constatin Mudende amesema wamekuwa wakitumia Mawakala wa pembejeo kufikisha mbole vijijini lakini baada ya mfumo huo kusitishwa kwasasa mawakala waliopo hawakidhi mahitaji ya wakulima hasa maeneo ya vijijini.

Aidha katika hatua nyingine Bw.Mudende amewataka wakulima kupanda mazao yao kwa wakati katika kipindi hiki cha mvua za mwanzo ili kupata mazao ya kutosha.


Hata hivyo amewataka wakulima kufuata ushauri wanao pewa na maafisa ugani ili waweze kunufaika na kilimo.

Post a Comment

0 Comments