habari Mpya


Tottenham Yapokea Kipigo Kikubwa Mechi ya UEFA Champions League 2019/2020.

October 1,2019 kumechezwa mechi nane za hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Champions League 2019/2020, huku Tottenham Hotspurs  akifungwa rundo la magoli dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani, katika uwanja wa Tottenham Hotspurs.

 Magoli ya Joshua Kimmich dakika ya 15, Robert Lewandowski aliyefunga mawili dakika ya 45 na 87 pamoja na Serge Gnabry aliyefunga hart-trick dakika ya 53, 55, 83 na 88 na kuufanya mchezo umalizike kwa magoli 7-2, huku Spurs wakifunga mawili kupitia kwa Son Heung-Min dakika ya 12 na Harry Kane kwa mkwaju wa penati dakika ya 61 kunaifanya Tottenham Hospurs kuingia katika rekodi mbaya ya kupokea kipigo chao kikubwa cha kwanza katika historia yao ya kufungwa katika mechi yao ya nyumbani.

Post a Comment

0 Comments