habari Mpya


TAMISEMI yahimiza Wananchi Kujiandikishaji Hadi Oktoba 17, 2019.

Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo, amesema Mkoa unaongoza kwenye uandikishaji kwenye daftari la mpiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa November 24,2019 ni Mkoa wa PWANI, ambapo Mikoa DAR ES SALAAM, ARUSHA na KILIMANJARO uandikishaji wao uko chini ya asilimia 50.

Wananchi waliojiandikisha kupiga kura Serikali za Mitaa sasa wafikia asilimia 68 ya lengo kitaifa.

TAMISEMI yahimiza wananchi zaidi kuendelea kujitokeza hadi Oktoba 17, 2019 zoezi litakapohitimishwa iili wapate fursa ya kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Post a Comment

0 Comments