habari Mpya


Stendi Kuu ya Mabasi Ngara Yalalamikiwa Licha ya Ukarabati Mwaka 2013.

Bango la Kuhusu Ukarabati wa Stendi hiyo Kuu ya Mabasi Mjini Ngara mwaka 2013.

Baadhi ya Abiria na Madereva wanao tumia kituo kikuu cha mabasi mjini Ngara wilayani Ngara mkoani Kagera wameilalamikia Halmashauiri ya wilaya hiyo kwa kushindwa kukifanyia ukarabati kituo hicho cha mabasi ikiwemo ujezi wa Jengo kwa ajili ya kupumzika wasafiri.

Wakizungumza na Radio Kwizera, Abiria hao wamesema wanakabiliwa na ukosefu wa Jengo la kupumzikia wakati wakisubiri usafiri sambamba na  kuhifadhi mizigo yao huku Madereva wakisema kuwa kituo hicho cha Mabasi kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa huduma ya choo na kuziba kwa mitaro ya maji machafu.

Mwenyekiti wa kituo hicho cha Mabasi Bw.Johari Kuboko amekiri kuwepo kwa changamoto hizo ikiwemo kukosekana kwa jingo la kufikia abiria na huduma ya choo kufungwa bila kufuata utaratibu na kwamba licha ya kulifikisha suala hilo katika Halmashauri mpaka sasa hakuna kilicho fanyika
Pichani Hapa Ukarabati wa stendi hiyo ulifanywa na Kampuni ya FARE (T) LTD  mwaka 2013 na uligharimu jumla ya Shilingi Milioni 26.

Akijibu changamoto hizo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.Erick Nkilamachumu amesema tayari Halmashauri wameandaa bajeti ya shilingi milioni 20 kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021 ili kutengeneza miundombinu mbalimbali ya kituo hicho kikuu cha mabasi likiwemo jengo kwa ajili ya Abiria.

Post a Comment

0 Comments