habari Mpya


Soma Habari ya Saa 24 October 11,2019 Radio Kwizera FM -Ngara.

Source; RK: KM (Afya ya akili)
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
KASULU

Wagonjwa elfu 2 na 622 wenye matatizo ya afya ya akili katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma, afya zao zimeimarika baada ya kupata ushauri wa wanasaikolojia kambini humo.

Hayo yamebainishwa na Dr. Godlove Kanyonga ambaye ni msimamuzi wa kitengo cha afya ya akili kutoka shirika la Msalaba mwekundu kambini Nyarugusu, wakati akizungumuza katika maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani ambayo yamefanyika hapo jana kambini humo.

Dr. Kanyonga ameeleza kuwa, wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili wapo kwenye tabaka tofauti kwani wapo wanaotibiwa na wengine wanahitaji ushauri wa wataalamu.

Aidha, ameeleza kuwa kati ya wagonjwa hao elfu 2 na 622 waliopewa ushauri na afya yao kuimarika, wanaume ni 873 na wanawake ni elfu 1na 749 ambao wengi wao wamepata matatizo hayo kutokana na majanga waliyoyapata wakiwa nchini mwao.

Kutokana na hali hiyo, Dr. Kanyonga amewataka wakimbizi kambini Nyarugusu, kuachana na tabia ya kuwaficha watu wenye Matatizo ya akili nyumbani na badala yake wawafikishe kwenye vituo ili kupata msaada.

Source; RK: Gmika (WAFANYABIASHARA)
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
GEITA

Wafanyabiashara wa soko kuu Mjini Geita Mkoani Geita wameiomba serikali kuwaboreshea miundo mbinu ya soko hilo ili kuepuka athari wanazozipata kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo bidhaa zao kuharibika.

Wakizungumza na Radio Kwizera baadhi ya Wafanyabiashara katika soko hilo wamesema kwa sasa hupata hasara kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki kwao kufuatia vibanda wanavyotumia kutokuwa imara hali inayopelekea bidhaa zao kunyeshewa na mvua.

Pia wameiomba serikali kuwahamisha katika eneo hilo ama kuwaboreshea miundombinu ili kuendena na bidhaa wanazouza kwa lengo la kuepuka hasara wanazozipata.

Hivi karibuni, mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinaly amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaendela kuimarisha miundombinu ya masoko ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi milioni 800 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa soko la Mbagala huku ujenzi wa soko jingine katika mtaa wa Nnyankumbu ukitarajiwa kuanza.

Source; RK: AE (Usalama)
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
KIGOMA

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General mstaafu Emmanuel Maganga amesema asilimia 40 ya wakazi wa mkoa wa Kigoma ni raia kutoka nchi jirani za Burundi na DRC jambo ambalo limekuwa likichangia uwepo wa matukio ya kiuhalifu

Brigedia Maganga amesema hayo katika kikao kazi cha kujadili usalama wa nchi tatu za Tanzania, Burundi na DRC kinachoendelea mkoani Kigoma kwa na lengo la kuimarisha usalama mipakani pamoja na namna ya kukabiliana na wahalifu wanaotoka katika nchi hizo

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zinazopakana na mkoa wa Kigoma katika kudhibiti matukio ya uvunjifu wa amani yanayojitokeza mara kwa mara katika maeneo ya mipaka inayozitenganisha nchi hizo na mkoa huo

Kwa upande wake kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Burundi Melchiades Rucheke amesema jeshi lake litahakikisha linatoa ushirikiano katika kuimarisha usalama na kwamba nchi ya Burundi haiko tayari kuona matukio ya uvunjifu wa amani yakiendelea kutokea huku akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa Mhimiri mkubwa wa kuchochea amani kwa nchi hiyo

Aidha kikao kazi hicho kimewakutanisha mkoani Kigoma wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda ambao wanajadili namna ya kuboresha masuala ya ulinzi na usalama katika mipaka inayotenganisha nchi hizo.

Source; RK: BF (Mgogoro)
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
NGARA

Diwani wa kata ya Ngara mjini wilayani Ngara mkoani Kagera Marton Gwihangwe amemtaka Afisa tarafa ya Nyamiaga Bw. Dadley Jackson Bahemu kupitia kwa haraka ripoti ya uchunguzi iliyowasilishwa na uongozi wa kitongoji cha Murugwanza Kati kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wawili wanaogombania eneo la shule ya msingi Murgwanza.

Bw. Gwihangwe ametoa kauli hiyo mara baada ya mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa mipaka ya shule Bw. Renatus Aloyce kusoma mbele ya wananchi na viongozi wa kitongoji taarifa juu ya uchunguzi uliofanywa kuhusu mgogoro huo.

Naye Afisa tarafa ya Nyamiaga Bw. Dadley Jackson amesema atahakikisha mgogoro huo unatatuliwa hataka ili kuweka wazi nani mmiliki halali wa eneo hilo

Wanaohusika na mgogoro huo ni Bw. John Clement na Bw. Zedek Ndabyanania ambao wote wanagombania eneo la uwanja wa umeme karibu na shule ya msingi Murgwanza na mgogoro huo umedumu kwa muda wa mwaka mmoja sasa.

Baadhi ya waliohudhuria mkutano huo, wamesema wanatambua eneo hilo ni mali ya shule hivyo taarifa iliyowasilishwa ni ya kweli

Source; RK: Amos J (Shule ya msingi yakabiliwa na changamoto ya miundo mbinu) 
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
SHINYANGA

Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo inakabiliwa na Msongamano wa Wanafunzi kutokana na uhaba wa Miundombinu ya Madarasa na Madawati katika shule hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Paul Kakema wakati akitoa taarifa ya changamoto zinazo ikabili shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi elfu 1 na 647 ambapo wanatumia vyumba 17 pekee vya madarasa

Hata hivyo Mwalimu Kakema ameeleza kuwa Licha ya uwepo wa changamoto ya miundo mbinu, bado shule hiyo inakabiliwa na upungufu wamadawati 50 hali inayopelekea wanafunzi kukaa kwa kubanana huku wengine wakikaa chini

Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wanaosomesha watoto wao katika shule ya Msingi Mwenge, wameomba serikali kukarabati miundo mbinu ili wanafunzi wapate sehemu nzuri ya kujifunzia.

Source; RK: TH {WATUMISHI  SITTA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI}
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
UKERWE

Jeshi la polisi Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza linawashikilia watu sita akiwemo mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo kwa tuhuma za wizi wa dawa za hosipitali zenye thamani ya shilingi milioni 400 ambazo zimeingizwa kinyemela kwa kutumia mifumo isiyo rasmi.

Zaidi ya milioni 881 za halmashauri hiyo zinatajwa kufanyiwa ubadhilifu ikiwa ni pamoja na kuibiwa kwa dawa ambazo zimeingizwa kwa mfumo usio rasmi huku muweka hazina wa halmashauri hiyo na mkusanyaji wa mapato wakituhumiwa kwa upotevu wa milioni 481.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe amesema mbali na kushikiliwa watu hao, kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo haiwezi kuvumilia ubadhilifu huo.

Kufuatia matukio hayo Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe ametoa siku 14 kwa muhasibu wilayani humo kurudisha fedha hizo ambapo kwa miaka minne mfulilizo watu hao wamekuwa wakifanya ubadhilifu wa fedha za halamsauri hiyo.


Source; RK: AG (Kichaa kuongezeka)
ED: AG
Date: Friday, October 11, 2019
BUJUMBURA

Idadi ya wagonjwa wa akili imetajwa kuongezeka Mkoani Gitega kaskazini mwa Burundi pamoja na mikoa jirani.

Kwa mujibu wa madaktari wa magonjwa hayo mkoani Gitega, kuanzia mwaka 2011 hadi 2019 wameshapokea nakutibu wagonjwa wa akili elfu tatu na mianane thamanini.

Taasisi ya URUKUNDO iliyopo mkoani Gitega inayaotibu magonjwa ya kuchanganyikiwa, inasema idadi hiyo ni kubwa na kwamba ugonjwa unaongezeka kwa sababu baadhi ya wananchi wanaamini ushirikina.

Mratibu wa taasisi hiyo, Bw. Mutawa Welazi Ndemeye amewashauri watu wenye magonjwa ya akili mkoani Gitega pamoja na mikowa jirani kupeleka wagonjwa wao katika taasisi hiyo ili watibiwe.

Post a Comment

0 Comments