habari Mpya


Rais Magufuli Afanya Uteuzi NEC, Ahamisha Wakurugenzi.

Rais Dkt. John Magufuli , Oktoba 1, 2019,  amefanya uteuzi na kuwahamisha kutoka vituo vyao vya  kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya na kuteua Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,  na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol).

 Katika uteuzi huo, amemteua Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).  Kabla ya uteuzi huo Dkt. Charles alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Pia amemteua Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo  Kanali Ibuge anachukua nafasi ya Balozi Grace A. Martin ambaye atapangiwa majukumu mengine ya kibalozi.

Aidha Viongozi  hao walioteuliwa akiwemo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi wameapishwa. 
Post a Comment

0 Comments