habari Mpya


Ngara-Ahukumiwa Miaka Mitano Gerezani Kwa Kosa la Kuishi na Mifupa ya Binadamu.

Kijana Charles Cornel Mkazi wa kijiji cha Kabalenzi kata ya Kanazi wilayani Ngara Mkoani Kagera amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kosa la kuishi na mifupa ya binadamu ikiwemo fuvu la kichwa nyumbani kwake.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Ngara Bw. Frendinard Kiwonde amesema Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 32 anastihili adhabu hiyo kwani kuishi na mifupa ya binadamu ni kinyume cha sheria.

Awali Mwendesha mashitaka wa Polisi Bw.  Jumanne Maatu aliiambia mahakama kwamba, kijana Charles Cornel alikamatwa Septemba 24 mwaka huu akiwa nyumbani kwake.

Post a Comment

0 Comments