habari Mpya


Matokeo ya Mechi za Klabu Bingwa Ulaya October 02,2019.

FC Barcelona ya Hispania usiku wa October 02,2019 katika uwanja wa Nou Camp waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Inter Milan kwenye hatua ya makundi ya UEFA Champions League 2019/2020 baada ya mchezo wao wa kwanza kutoka sare ya 0-0  dhidi ya Borussia Dortmund.

Katika mchezo huo FC Barcelona walianza vibaya kwa kujikuta wakiruhusu kufungwa goli la mapema la Inter Milan dakika ya pili kupitia kwa Lautaro Martinez lakini mambo hayakuwa mazuri kwa Barcelona hadi walivyoingia kipindi cha pili.

Luis Suarez ndio alikuwa mkuki wa sumu wa Inter Milan kwani alifunga goli la kusawazisha dakika ya 58 na kufunga goli la ushindi dakika ya 85 na kuufanya mchezo umalizike kwa Barcelona kupata ushindi wa 2-1, Lionel Messi akiibuka kidedea kwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi (6) kuliko mchezaji yoyote katika mchezo huo, Barcelona sasa wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point 4 katika kundi lao sawa na Dortmund ayeongoza wakati Inter Milan na Slavia Praha wakiwa na point moja moja kila mmoja.

Post a Comment

0 Comments