habari Mpya


Kijana Mbaroni kwa Kuoa Mwanafunzi wa Sekondari Ngara.

Na Simon Dioniz – RK Ngara.

Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera linamshikilia kijana Dickison Joasi mkazi wa kitongoji cha Murugando kijiji cha Kumtana kata ya Kibimba baada ya kukutwa akiwa amemuoa mwanafunzi wa shule ya sekondari anayesoma kidato cha pili.

Kijana huyo mwenye miaka 31 amekamatwa alfajili ya October 24,2019 na Mgambo wa kijiji kwa kushirikiana na afisa Mtendaji wa kijiji pamoja na mzazi wa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Nassor John Baloga.

Mkuu wa Polisi wilayani Ngara Bw. Abeid Maige amesema Mtuhumiwa leo October 25,2019 anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Mzazi wa mtoto wa kike Bw. Nassoro John Baloga amesema kuwa alipopata taarifa za mwanae kuwa ameolewa na hahudhurii masomo aliweka mtego kwa ajili ya kumnasa ambapo amekutwa akiwa amelala kwa kijana huyo na alikuwa ameishi naye kwa zaidi ya wiki mbili.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa kijiji cha kumtana wamelaani kitendo hicho na kueleza kwamba shule ya Sekondari Kibimba imekuwa ni eneo la kukuzia watoto kwani Mimba ni nyingi ukilinganisha na maeneo mengine ya wilaya ya Ngara.

Post a Comment

0 Comments