habari Mpya


Kagera Sugar Yakabana Koo na Namungo FC Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Timu ya Kagera Sugar Jana October 24, 2019 imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara 2019/2020 uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Ushindi huo unaifanya Kagera Sugar ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi saba, ikijikita hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu sasa ikilingana na Namungo FC inayoshika nafasi ya pili.

Kagera Sugar inayofundishwa na Kocha Mecky Mexime  ilifunga magoli yake kupitia kwa  Erick Kyaruzi dakika ya 17, Yusuph Mhuli dakika ya 27 , Frank Ikobela dakika ya 31 na Geofrey Mwashiuya kuifungia Kagera Sugar bao la nne dakika ya 60.

Bao pekee la Mbeya City lilifungwa na Mohammed Mussa dakika ya 35 akimalizia pasi ya Frank Damas.

Post a Comment

0 Comments