habari Mpya


Elimu kwa Wataalamu wa Sekta ya Afya Kigoma Yatolewa Kujikinga na Maambukizi (magonjwa).

Na WAMJW - KIGOMA.

Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kitengo cha Uhakika Ubora inaendelea na kutoa elimu kwa Wataalamu wa Sekta ya Afya ngazi ya Mkoa (RHMTs) na ngazi ya Wilaya (CHMTs) juu ya namna bora ya kujikinga dhidi ya maambukizi (magonjwa) ikiwemo ugonjwa wa Ebola wakati wa kutoka huduma Mkoani Kigoma.

Elimu hii inaendelea kutolewa katika mikoa yote iliyo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako mlipuko unaendelea. 
Hata hivyo, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imekwisha kuchukua hatua mbali mbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwamo kuelimisha Jamii njia za kujikinga dhidi ya ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea. 
 
Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Management Science for Health (MSH) kupitia mradi wa Medicines, Technology and Pharmaceutical Services (MTaPS), yanatarajia kuendelea katika mikoa yote iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini. 
 

Post a Comment

0 Comments