habari Mpya


Bilioni 3 Kujenga Miradi ya Maendeleo Ngara Chini ya NELSAP.

Moja ya Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vitatu vya Madarasa ulipokaguliwa na Kamati ya Fedha ya Halmashauri wilayani Ngara katika ukaguzi wa vyumba hivyo Shule ya Sekondari Lukole.

 Picha Na -NGARADC.
Zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeanza kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Ngara Mkoani Kagera inayofadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya usimamizi wa shirika la NELSAP inayofanyika kwenye vijiji wilayani humo. 

Mratibu wa Miradi hiyo Bw. Herman Hume amesema baada ya mchakato wa kutafuta wakandarasi wiki hii wamekabidhiwa maeneo ya ujenzi ambapo wamekabidhi kuanza ujenzi wa kituo cha Afya Lukole ambapo watajenga majengo 7.

Aidha Maeneo mengine ni ujenzi wa madarasa shule ya Sekondari Rusumo, Shule ya Msingi Kyenda, Shule ya Sekondari Bukiriro na Shule ya msingi Mukubu .
Hata hivyo amesema miradi mingine ambayo iko kwenye hatua za kukamilisha manunuzi ni pamoja na mradi mkubwa wa maji kata ya Rusumo ambapo vijiji vyote vya kata hiyo vinatarajia kunufaika na mradi huo ambao utatoa maji kutoka  mto Ruvubu.

Post a Comment

0 Comments