habari Mpya


Basi la Abood Lapata Ajali Leo Dar Es Salaam.

Basi la abiria mali ya Kampuni ya Abood Bus Services Ltd, limepata ajali leo October 30, 2019, Eneo la Kimara Temboji, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa, basi hilo lilikuwa likitoka Stendi ya Mabasi, Ubungo , kupitia Barabara ya Morogoro, baada ya dereva wa basi hilo kugonga gema, lilipolekea taili la basi hilo kupinda na kwamba hakuna abiria yeyote alijeruhiwa.
Akizungumzia ajali hiyo leo Oktoba 30, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi, huku chanzo akikitaja kuwa ni wembamba wa barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo katika upanuzi , kwahiyo Dereva katika kuingia, aliingia vibaya na tairi likalala na kupelekea Basi likainama”.
 

Post a Comment

0 Comments