habari Mpya


Wasimamizi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kagera Wala Viapo Vya Uaminifu, Utii na Uadilifu.

Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoani Kagera walioteuliwa na kuapishwa rasmi Septemba 12, 2019 ni Bw. Richard Masanilo Mihayo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Bw.Bablyus Lubingo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Bw. Albert Mamimo Msemwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bw. Rajab Khasim Byoma Halmashauri ya Wilaya Karagwe.
Wengine ni Bw. John Mayuga Msafiri Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Bw. Lucas Haga Daudi Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Bw. Costantino Francis Msemwa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo na Bi Essery Felician Pima Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 ambapo Wasimamizi wa Uchaguzi huo Katika ngazi za Halmashauri za Wilaya nane za mkoa wa Kagera,wameapishwa na kula viapo kusimamia uchaguzi huo.


Wasimamizi hao nane walioteuliwa rasmi Septemba 11, 2019 na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo na wakila viapo vya uaminifu, utii na uadilifu mbele ya Mhe. Flora Kaijage Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Bukoba Septemba 12, 2019 na kuwa wasimamizi rasmi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa Mkoa Kagera.

Post a Comment

0 Comments