habari Mpya


Mtihani Darasa la Saba 2019 Ngara-Walimu 10 Mbaroni kwa Wizi.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi.

Walimu  watano wa shule ya Msingi Kumunazi, Kata ya Kasulo  na Walimu  watano kutoka katika shule mbali mbali za Msingi wilayani Ngara Mkoani Kagera wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za  kujihusisha  na uvujishaji mtihani wa  taifa wa darasa la saba uliofanyika septemba 11 na 12 mwaka huu,2019.

Akizungumza Septemba 13, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema  Walimu hao walikamatwa September 12,2019  baada ya kupata taarifa za wasimamizi  waliokuwa wanasimamia mtihani kwa kushirikiana na Walimu wa shule hiyo  kuwa waliwafanyia na kuwapa  majibu ya mtihani wa    somo la Sayansi.

Walimu waliokamatwa wa shule ya msingi Kumunazi ni pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Manase Mitinange, Prosiper  Pius,  Johakimu Kakuru,  Kilistian Ileta,  na Erick Baribate.

Aidha Walimu wengine waliokuwa wakisimamia mtihani huo wa darasa la saba 2019 waliokamatwa ni pamoja na Roevokatus  Juhudio  kutoka Shule ya Msingi  Kasharazi,  Jerusa Mganga kutoka Shule ya Msingi  Nyakahanga, Rusulo Isaka kutoka Shule ya Msingi  Kasharazi, Godfrey Mashaili kutoka Shule ya Msingi Mayenzi na Heziron  Eugo kutoka Shule ya Msingi  Mikole.
Aidha Kamanda Malimi amesema, bado wanaendelea na upelelezi na pindi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.

Post a Comment

0 Comments