habari Mpya


Anashikiliwa na Jeshi la Polisi Geita Kwa Tuhuma za Kuishi Kinyumba na Binti yake wa Miaka 16.

Mji wa Geita.
Mwanaume Joseph Masalangulu miaka 36 mkazi wa kitongoji cha Mabamba Mkoani Geita anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuishi kinyumba na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 16 mwanafunzi wa darasa la sita.

Akizungumzia na radio kwizera mtoto huyo amesema baba yake amekuwa akimlazimisha kufanya naye mapenzi pale mama yake anapokuwa hayupo nyumbani.

Mwenyeikiti wa serikali ya kijiji cha Inyara Bw.Elisha Maige na Kaimu afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Manumbu Thomas wamekiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa amekamatwa kwa ushirikiano na wananchi na kumkabidhi katika kituo cha polisi Katoro.

MAJIRANI WA TUKIO HILO.

Kamanda wa polisi Mkoani Geita Mponjori Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Post a Comment

0 Comments