habari Mpya


Wengine 6 Wafariki Ajali ya Moto Morogoro.

Ajali ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro inaendelea kugharimu maisha ya watu na hivi sasa waliofariki kutokana na mkasa huo wa Jumamosi August 10,2019  asubuhi wamefikia 82.

Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi sita kati ya wale waliolazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuaga duni.

Watu 62 walithibitishwa kufariki siku ya mkasa na zaidi ya 70 kujeruhiwa na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu.

Awali idadi ya majeruhi 46 walisafirishwa kutoka mkoani Morogoro mpaka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya kibobezi.
Mpaka kufikia August 14, 2019, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bw Amini Algaesha amesema idadi ya majeruhi waliosalia hospitalini hapo ni 32, kati yao 17 wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi wakiendelea kupatiwa matibabu.

MSIKILIZE HAPA CHINI.


Katika kukabiliana na athari ya janga hilo kwenye jamii, serikali ya Tanzania imetuma timu ya wataalamu wa ushauri, saikolojia na ustawi wa jamii mjini Morogoro kwenda kuwahudumia wale waliopoteza ndugu na jamaa ama kupata majeraha.

Kiongozi wa msafara huo wa wataalamu takribani 30, Dkt Naftali Ng'ondi kutoka Wizara ya Afya Tanzania ameiambia BBC kuwa timu yake ipo Morogoro tangu Jumatatu Agosti 12.

Baadhi ya matukio ya mikasa ya malori ya mafuta Afrika
  • January 31 2009 Kenya: Moto uliwachoma watu waliokuwa wakifyonza mafuta wakati lori la mafuta lilipoanguka huko Molo kaskazini mwa mji wa Nairobi na kuwaoa watu 122.
  •  
     
  • Julai 2, 2010, DR Congo: Takriban watu 292 waliuawa wakati lori la mafuta lilipolipuka mashariki mwa kijiji cha Sange. Baadhi ya waathiriwa walikuwa wakijaribu kuiba mafuta baada ya ajali hiyo huku wengine wakitazama mechi ya kombe la dunia.

  • Oktoba 6, 2018 DR Congo: Takriban watu 53 waliuawa baada ya lori la mafuta kugongana na gari jingine na kushika moto katika barabara kuu ya mji mkuu wa Kinshasa.

  • Septemba 16 2015 Sudan Kusini: Watu 203 walifariki na wengine 150 kujeruhiwa wakati watu walipokuwa wakijaribu kuiba mafuta.

  • Novemba 17 2016 Msumbiji: Takriban watu 93 waliuawa wakati lori la mafuta lililokuwa likibeba petroli lilipolipuka magharibi mwa taifa hilo . Mamia walikuwa wakijaribu kufyonza mafuta kutoka katika gari hilo.

  • Julai 12 2012, Nigeria: Takriban watu 104 walifariki walipokuwa wakijaribu kuchukua mafuta kutoka kwa lori la mafuta baada ya kuanguka kusini mwa jimbo la River State.
  • Oktoba 9 2009 , Nigeria: Takriban watu 70 walifariki kusini mashariki mwa jimbo la Anambra baada ya lori la mafuta kulipuka huku moto ikichoma magari kadhaa.
BBC Swahili/Radio Kwizera.

Post a Comment

0 Comments