habari Mpya


Kagera Yazindua Rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji.

Nimehudhuria makongamano ya uwekezaji katika mikoa sita lakini kwa mkoa wa Kagera kweli mmejipanga kuhamasisha uwekezaji maandalizi yenu si ya michezo mnaye mkuu wa mkoa mbunifu na mfatiliaji, nimepita kwenye mabanda nimejionea bidhaa mbalimbali zinazosindikwa hapa Kagera kweli Kagera kwa mkakati huu mtafanikiwa.


Maneno hayo yalisemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera Agosti 14, 2019 katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba alipokuwa mgeni rasmi na kuzindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera amesema kama mkakati wa Wiki ya Uwekezaji Kagera utatumika vizuri utaleta hamasa na uwezo wa kiuchumi wa mwananchi mmoja mmoja, uwezo wa mkoa pia na Taifa kwa ujumla huku akiwataka Watanzania wenyewe wawe mstari wa mbele kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo ili kuharakisha maendeleo.

 MSIKILIZE HAPA

Akiwasilisha taarifa ya Mkoa juu ya fursa za uwekezaji mkoani humo, Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti amesema Kagera inawakalisha ukanda wa Kasikazini Magharibi kwa fursa ulizonazo na kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na kwamba bado yapo maeneo mengi ya uwekezaji ambayo hayajawekezwa na yakipata wawekezaji yatakuza uchumi wa nchi.

MSIKILIZE HAPA RC GAGUTI
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Mhe.Innocent Bashungwa amesema Wizara yake imeanza kuondoa vikwazo vyote vya kibiashara vilivyokuwa vikiwakwamisha Wananchi kuwekeza kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na itaendelea kuweka Mazingira wezeshi kwa wawekezaji kufanya shughuli zao.

SAUTI YA WAZIRI BASHUNGWA
Mara baada ya hotuba yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alizindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera , pili alizindua Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera na alizindua rasmi Kongamano la kujadili na kudadavua fursa za uwekezaji Kagera ambalo litaanza rasmi leo August 15, 2019  huku wakati wote huo maonesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba.

Post a Comment

0 Comments